Tanzania's Trusted Car Marketplace

Ni nani atakaenililia siku nikifa?

Huenda umewahi kukutana na swali hili: "Ni nani atakaelia siku nikifa?"

Si swali ambalo ningependa kulifikiria sana. Hakuna anayependa kufa. Licha ya vitabu vya dini kutukumbusha kwamba dunia si makazi yetu ya milele, wengi wetu bado hatutamani kuondoka. Si tu sababu tunapenda dunia na vitu vyake kupita kiasi, bali kuna sehemu ndani yetu inayotamani kuendelea kuishi, kuwa na muda zaidi na watu tunaowapenda, na kuona mambo ambayo bado hatujayaona.

Lakini yote kwa yote, kifo kipo. Hakichagui umri, rangi wala utajiri. Tajiri kwa maskini, kijana kwa mzee, sote tutakufa siku moja.

Swali ni: Ni nani atakayelia siku ukifa?

Pamoja na kwamba sote tutakufa, ni wazi kwamba hatutaliliwa na watu sawa. Wengine wataombolezwa na familia zao pekee. Wengine wataombolezwa na familia, marafiki na jamii nzima. Na huenda wapo watakaoondoka duniani bila mtu yeyote kutambua kuwa wameondoka.

Kama ilivyo kwa binadamu, ndivyo ilivyo pia kwa biashara.

Je, ni nani atakayelia siku Wavuka tukifa?

Centered

Wavuka ni soko la magari nchini Tanzania. Kama ilivyo katika masoko mengine, utakutana na magari mbalimbali, kutoka maeneo tofauti na kwa wauzaji tofauti nchini Tanzania.

Wavuka ipo kwa ajili ya kurahisisha biashara ya magari. Inampa mmiliki binafsi wa gari nafasi ya kutangaza gari lake na kulifikisha kwa watu wanaoweza kuwa wanunuzi. Vilevile, wafanyabiashara wenye ofisi na biashara rasmi za magari wanapata nafasi ya kuonyesha magari yao na kuwafikia wateja wengi zaidi.

Vivyo hivyo kwa wanunuzi, wananaweza kutumia Wavuka kulinganisha bei za magari nchini, kuona chaguzi mbalimbali na kupata picha ya uhalisia wa soko la magari yanayopatikana sokoni kwa wakati husika.

Hivyo basi, siku Wavuka tukifa, tunaamini kwamba wapo watakaotulilia. Wapenzi wa magari, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, wanaume kwa wanawake, madalali na mafundi wanaoamini katika soko lenye uwazi na ushindani.

Hatutarajii kufa leo wala kesho bali mbele tunaendelea ili kuhudumia jamii na kuwa sehemu muhimu ya soko la magari nchini Tanzania. Lakini siku moja, tukifika mwisho wa safari yetu, tunatumaini kwamba tutakuwa tumeacha alama ambayo watu wataikumbuka.

Kabla hatujafika siku hiyo, tuna kazi ya kufanya. Kazi ya kujenga soko ambalo linawanufaisha wanunuzi na wauzaji, na kufanya biashara ya magari iwe rahisi na yenye uwazi zaidi.

Discussion
0

Be the first to comment.